Yanga yamtambulisha winga wake wa kushoto Skudu kutoka Marumo Gallants

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Hatimaye Club ya Yanga imefanikisha kunasa saini ya mchezaji kinda kutoka Afrika Kusini anayeitwa Mahlatsi Makudubela (33) almaarufu kama Skudu.


Mchezaji huyo kinda (33) alikuwa anakipiga kwenye timu ya Marumo Gallants ya Afrika kusini iliyofika nusu fainali kombe la shirikisho Africa.


Kwa sasa Club yake ya zamani imeondolewa ligi kuu huko Afrika kusini kutokana na kutofanya vizuri na kusababisha ishuke daraja.


Mwana nusu fainali huyu alizua gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kutoka na tetesi zake za kujiunga na miamba ya Soka ya Jangwani.


Club ya Yanga imempa jezi namba 6 winga huyu na anatarajiwa kufanya makubwa sana.


Hii ni replacement nzuri ya Morrison.


 
 
Back
Top Bottom