Duru za siasa: Uchaguzi ni juu ya ilani/sera na hatma ya nchi

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
UTANGULIZI


Uchaguzi ni tukio la kidemokarasia la kuchagua au kuchaguliwa kupata watakaokupewa madaraka


Si tukio la kupata ''watawala'' bali viongozi watakaotumikia wananchi


Ni muhimu kuwajua wenye madaraka kwa hulka na tabia, maono, na wanachosimamia kupitia vyama vyao tu


Ni haki kwa wananchi kuwajua wagombea nafasi mbali mbali kwa hulka, tabia, na wasifu.


Ni muhimu kujua ilani/sera walizopewa si kwa maandishi bali wanavyozitafsiri na kuzijengea hoja. Tutalitolea mfano mbele


Nchi masikini zinazokumbatia demokrasia ya kujfiunza tunachagua viongozi kama watu, kwa muonekano na ubabaishaji wao


Tawala za kiasili za machifu zilizingatia mrithi wa kiti kwa tabia, maono, unyenyekevu na sifa za uongozi.


Aghalabu, mrithi mtaraJiwa angeweza kuachwa kwa sababu tu hakidhi vigezo na si kuwa ndiye mrithi anayefuata


Na wala si kwa Afrika tu, Uingereza ilishatokea mfalme ‘akaachia ngazi' (King Edward VIII 1936-Abdication)


Kwa Waafrika limekuwa tatizo. Tunaangalia mambo yasiyo na umuhimu kuliko tunayopaswa kuyatolea uamuzi kweye kura


Nchini, mijadala imetawaliwa na hisia, fitna, majungu n. K.


Tumeusahau ilani/sera zitakazotumika ‘kutusaidia au kutuhukumu' Mwisho tunavuta viti na majamvi tukilalamika.


Tuliowapa madaraka kwa upuuzi wetu wa ‘homeboy' au kabila, kanda na dini wanajilimbikizia


Mwishowe kutuporomoshea mitusi wanapo mnadi mlinzi wa malimbikizo anayefuata. Si wao ni sisi wajinga, hatukuangalia


Ni kwa msingi huo, tunaona umuhimu wa majadiliano kuhusu wagombea na ilanisera.


Bila kufanya hivyo tutarudi kujiuliza inakuwaje tuliwachagua wakiwa hawajui kwanini sisi ni masikini.


Tutajiuliza kwanini umasikini unatopea badala ya kupungua.


Tutabaki taifa mahiri la walalamikaji, na la wazembe wa kufikiri


Tunaangalia kwa fikra katika mabandiko yajayo


Inaendelea….


 
 
Back
Top Bottom