Duru za Siasa: Marekani (U. S) Chini ya Donald J. Trump

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Wanajamvi


Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D. J Trump kuwa Rais wa 45

Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US


Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi

Siasa za Marekani, taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani


Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo


Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu

Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani


Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani


Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu


Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwa sababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa, uchumi, jamii n. K. Trump ndiye Rais wa Marekani


Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi


Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake


1. Maandamano ya wanawake duniani

2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)


Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni


Tusemezane


 
 
Back
Top Bottom