Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
ELECTION NIGHT IN AMERICA


Ref: Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA


H. CLINTON (DEM) VS D. TRUMP (GOP)


Wanajamvi

Miaka, miezi, siku na ni masaa machache tu uchaguzi wa Marekani utakamilika.


Macho ya dunia yapo Marekani kujua nani atakuwa Rais ajaye wa Taifa hilo lenye nguvu


Uchaguzi wa Marekani unaathari kubwa kwa dunia. Ni taifa lenye nguvu za kiuchumi, kijeshi, kisiasa na kijamii zinazoathiri mataifa mengine. Kwa hali yoyote ni tukio linalogusa dunia


Hatua zote za uchaguzi zimefanyika na upigaji kura wa awali umeshamalizika


Kesho ni siku ya kupiga kura ambapo state zilizokuwa na uchaguzi wa awali zitamalizia na zile zinazofanya kea siku moja zitamaliza.


Itakapofika saa 3.0 usiku saa za Marekani sawa na saa 11 saa za Tanzania vituo vya mashariki vitafungwa. Vituo vya Marekani kati na magharibi vitafunga kwa muda huo kwa nyakati zao


Kwa kuangalia ramani ya uchaguzi na umuhimu wa Mjaimbo, matokeo yanaweza kukamilika ikifika saa 4 au 5 za Marekani kama hakutakuwa na tatizo ambazo ni sawa na saa 12 au 1 za Tz


Uzi huu utakuwa maalumu na endelevu ukiwaletea hali halisi ya matokeo kwa muda (real time)


Kutakuwa na uchambuzi wa kila tukio linalohusiana na uchaguzi kwa wakati


Nyote mnakaribishwa na uzi huu utakuwa 'active' kesho Jumanne saa 2 za usiku za Marekani sawa na saa 10 usiku Tz na kuendelea hadi matokeo ya mwisho


Hadi wakati huo endelea kuwa nasi Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA


Kaa mkao wa habari


 
 
Back
Top Bottom