Unawekeza Tsh 30m unapata kodi 300k kwa mwezi. Mwenzio kawekeza Tsh 2m anapata hiyo hiyo

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Dah nazidi kujifunza wakuu, nazid kujifunza.


Ujue sisi ambao tulikuwa tumesoma ma kozi magum magumu huku kwenye ulimwengu wa biashara huwa wengi hatuko vizuri lakini ukijipa muda ukakubali kufundishika aisee.


Usinambie ooh hiyo mbona hesabu rahisi tu ndiyo utekelezai sasa


Na huo ni mfano tu, kuna scenario nying tu.


Unafungua ka mini supermarket kazuuuri umetumia labda Tsh8m kwa mwezi faida labda 800k. Mwenzio hapo hapo pembeni ana genge katumia mtaji wa Tsh 2m or Tsh 1m anakukunjia faida 1m monthly.


Aisee kuna visheria vya biashara sisi ambao hatuna misingi ya elimu ya business inabidi tukubali kujifunza.


Naamini ukifuata taratibu za kibishara unatoboa vizuri tu.


Naendelea kujifunza tena na tena.


Uzi umeandikwa baada ya kuwa inspired na mzee mmoja hivi nimepita ofisini kwake leo Mwenge hapo.. Dah.. Mzee huyu ana nyumba kama 40 hivi ananambia mwanangu ningekuwa na knowledge enzi hizo kama niliyokuwa nayo sasa kuhusu biashara ningekuwa mbali sana.


Anasema yeye alikuwa anajenga majumba tu anapangisha, anawekeza hata Tsh 100m nyumba ambayo mwisho wa siku kodi analipwa lets say 700k wakai kwa sasa fremu yake ya biashara moja tu yenye mtaj wa lets say Tsh 15m inamuingizia faida ya mpaka Tsh 1m weekly.


Anasema anawish hizo nyumba mtaji wote huo angeugawa huku tho now ana frem zaidi ya 50 Dar pekee bado mikoani. Huyu mzee ni bilionea ila ukimkuta kwenye maduka yake huwezi gundua.


Ndiyo anaweza kopea mikopo hizo nyumba ila yeye mwenyewe anasema kuwekeza kwenye majumba ni biashara kichaa na ya woga.


Uzi tayari.


 
 
Back
Top Bottom