Tuliowahi kukopa pesa kuanzisha biashara kisha biashara ikafa tukutane tujadili machungu

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Sitausahau mkopo wangu wa kwanza kabisa. Ndipo nilipoanza kushika mamilioni, ilikuwa September 2016. Basi nikanunua kiwanja kimoja na pesa nyingine nikaiingiza kwenye biashara ya duka la vitu mchanganyiko.


Aisse biashara ilinikataa kabisa. Duka la milioni kadhaa mauzo elfu 20 per day. Mwisho wa siku Mimi ndiye nikawa nalilisha duka badala ya Mimi kulishwa na duka.


2017 nikakopa tena huenda nitainuka nikaambulia hola nikamkumbuka wife aliyenishauri nisiiingize ile fedha dukani. Nikafunga biashara. Hapo ndipo nikaanza kuwa huru.


Ile pesa ni heri ningenunua mbwa niwafuge aisee, inaniuma mpaka kesho.


Nimeweza kufanya maendeleo maada ya kuacha business.


 
 
Back
Top Bottom