Siri Ya Hati Ya Muungano Na Njama Za Kuuficha

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Mjadala huu utakuwa na sehemu kuu NNE.


SEHEMU YA KWANZA: Msingi Wa Mkataba Ulikiukwa, Woga Wa CCM Serikali Tatu.


Mchakato wa Katiba Mpya ulitoa fursa pekee kwa CCM kurekebisha kasoro zilizojitokeza huko nyuma ambazo ndiyo zimezaa "kero sugu" za muungano. Iwapo CCM ingekiri makosa hayo huku ikitoa sababu mbalimbali za kihistoria na mazingira ya dunia ya wakati ule kwa ujumla, wananchi wengi wangesema "Yaliyopita Si Ndwele, Tuyagange Yaliyopo na Yajayo". CCM ingepata fursa ya kuaminiwa na sehemu kubwa ya umma na kushirikiana na chama hiki katika uzinduzi wa Tanganyika.


Hii ilikuwa ni fursa adimu ya chama (CCM) kuhakikisha kwamba: (1) inarithisha vijana wake Chama ambacho kimemaliza kazi ya kulimaliza ‘jinamizi' lililosumbua chama na taifa kwa miaka zaidi ya 30; (2) Chama kinajenga mazingira ya kukomesha "Suala la muungano" kuwa ni "suala la vyama vya siasa" bali suala la "kitaifa"; (3) Chama kinalinda na kuboresha muungano kwa kufuata mapendekezo ya tume ya mabadiliko ya Katiba. Hatua ya chama kuendelea kutetea serikali mbili katika mchakato wa Katiba, ni sawa na kuamua kuendelea kulea Kero za Muungano, na siyo kuzipunguza kero hizi kama chama kinavyodai [rejea kauli za CCM za hivi karibuni kupitia Katibu Mkuu Taifa (Abdurahaman Kinana), na Katibu wa CCM NEC Taifa (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye].


Mkataba wa Muungano (1964) ulitoa sura ya kuwepo kwa shirikisho la serikali tatu [Masuala kumi na moja ya Muungano, huku masuala nje ya haya kumi na moja yakibakia kwa serikali za nchi shiriki za muungano (Yani Serikali Ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar)]. Chini ya mfumo huu wa serikali tatu, kati ya serikali hizi mbili shiriki (Tanganyika na Zanzibar), hakuna Serikali iliyopangwa na Mkataba wa Muungano kuwa na madaraka makubwa kuliko serikali nyenzake. Kilichobadilisha yote haya ilikuwa ni chama cha TANU kuingilia suala la muungano kinyume na mkataba wa muungano (1964).


MKATABA WA MUUNGANO: Vyanzo (Sources):


1. Jumbe, A (1995): The Partner - Ship: Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30 Ya Dhoruba.

2. Shivji, I (2008): Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika and Zanzibar Union.


Inaendelea bandiko linalofuata (#2).


Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Cc Nguruvi3, @FJM,@ Tpaul, @Mag3, @JokaKuu, @Mwigulu Nchemba, @Nape Nnauye, @MwanaDiwani,@Zomba, @Ritz, @ZeMarcopolo, @Gamba la Nyoka, @Mtanganyika, @Mzee Mwanakijiji, @Pasco, @Kitila Mkumbo, @EMT, @MTAZAMO, @Kobello, @Jasusi, @Zumbemkuu, @Mimibaba, @Zakumi, @Invisible, Kurugenzi ya Habari, @Mnyepe, @Yericko Nyerere, @FaizaFoxy, @Dingswayo, @Makusudically, @Tumaini Makene, @Nicholas, Mtu wa Pwani, Jmushi1, Mwita Maranya, Ngongo, Zumbemkuu, Mzawa Halisi, Barubaru, Mindi, Kiganyi, Communist


 
 
Back
Top Bottom