Nyumbani Lounge kwa JayDee huduma kwa mteja hairidhishi

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Wiki iliyopita niliyapitia maeeneo hayo ya Mwenzetu ambayo kwa kusema ukweli Bint amejitahidi sana sana, kwa bint kama yeye kutoka aliko tokea mpaka hapa alipofikia ni hadithi nzuri ya mafanikio ya yenye kutia moyo kwa mabint wengine na hata watu wajinsia nyingine.

Lakini, pamoja na yeye kama yeye kufikia mafanikio hayo sehemu yake ya chakula hiyo Nyumbani Lodge naona imepata au inapata umaarufu tu kwa kumpitia Jaydee na siyo kama sehemu nzuri na yenye hudumu nzuri.

Kwa huduma, hamna huduma nzuri kabisa... Yaani unaweza kukaa hapo baada ya kuagiza chakula zaidi ya saa nzima au mbili bila hatakuletewa chakula chenyewe na kila ukiuliza unaambiwa subiri, ukichoka kusubiri utaamua kuhairisha ulicho agiza kwa sababu ya kuchoka kusubiri huko na hata 'huto-ombwa'samahani ila wahudumu watendelea kujipitisha tu mbele kukufanya kama umeenda hapo kupewa chakula cha charity.

Ushauri wangu Dada jaydee nenda katafute wahudumu professionals wanao jua kazi yao na kuithamini vinginevyo utapoteza wateja na biashara kwa sababu ya ujinga ya hao wahudumu uchwara.


 
 
Back
Top Bottom