Nimenunua simu mtandaoni ikatumwa kwa posta leo nimeipata

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 2:01 AMReplies 0 · Views 0
#1
Habari wakuu niliagiza mzigo wangu wa simu tarehe 22/09 tarehe 23/09 ukatumwa kuja Tanzania kutokea china.

Juzi nilihofia kupoteza nikaandika na uzi humu

Nilitumiwa kwa njia ya posta mzigo ukaingia bongo tarehe 26/09 baada ya hapo ukatumwa kuja mpaka moshi nilipo kwa sasa siku ya ijumaa leo nimeenda posta nikaupata


Nimeagiza zaidi ya mara 40 na cjawah kuibiwa


Niliagiza kupitia mtandao wa aliexpress


Sijatozwa kodi wala chochote sijalipa hata mia.


MSIOGOPE KUNUNUA VITU MTANDAONI KUNA VITU VIZURI SANA HUKO EBAY, AMAZON, ALIEXPRESS NA ALIBABA


Huo ndo mrejesho wangu


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread