Naomba ushauri kuhusu network market ya Neolife

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Jamani naomba tu niwasalimu. Kuna changamoto moja naipata juu ya Neolife ni network market ambapo kuna mshikaji tunaheshimiana sana of course ni uncle ananilazimisha kujiunga nae. Anadiriki kunitukana kwamba utabaki maskini kama huoni fursa halafu pia yaani ananidharau.


Tatizo hata yeye siyo kivile katoboa life sana japo pia siyo poor kivile kwani ana hela ya kubadilisha mboga na nyumba mbili na vigari kama vitatu hivi.


Sasa changamoto hii Networking Hai-click kabisa kichwani kwangu, kwa jinsi bidhaa zilivyo na aina ya wateja inakuwa vigumu kwani ni lazima ujitangaze ili wanunue kwa jina lako upate points au uwaunganishe chini yako wanunue na kupanua mtandao ndipo ufaidi. For me naona ni ndoto.


Nimeamua kuwa quiet ili asinisumbue. Mungu ndiyo anapanga maisha ya mtu. Ushauri plse.


 
 
Back
Top Bottom