Naomba kufahamu kuhusu tatizo la mtoto kutozungumza mapema

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Habarini za weekend hii?


Tatizo langu ninaloliwasilisha hapa ni juu ya mtoto wangu kuwa mzito kuzungumza au kushindwa kunyoosha sentensi vizuri ili aeleweke kama ilivyo kwa watoto wengine.


Kwa sasa ana umri wa miaka mitatu (3), watoto wenzake hapa mtaani tunaoishi nao wao wanajua kuongea mpaka hata wale aliyowatangulia kiumri tayari wanajua kuongea kumzidi yeye. Hii hali mimi nimekuwa nikiiona ya kawaida tu, nikijua kuwa atajua kuongea kadri anavyozidi kukua.


Kilichonifanya mpaka kuja hapa kuomba msaada wenu wa ushauri au wa kitabibu ni juu ya mmama mmoja jirani yangu kuniambia mwanao ana kilimi, hivyo inamfanya ulimi kuwa mzito kuongea hali inayomfanya ashindwe kueleweka vizuri. Ameniambia nimpeleke hospital au nitafute mtu mzima mtaalamu wa mambo hayo amtibie.


Jamani naombeni ushauri juu ya hili, ili nichukuwe hatua mapema, maana nahitaji kumpeleka nursery mwezi wa 6.


Sent using Jamii Forums mobile app


USHAURI ULIOTOLEWA NA MDAU:


 
 
Back
Top Bottom