Naacha kazi serikalini

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Habari wakuu wote wa jf

Nawapenda sana hasa kwa mambo mazur nnayopata

Mmi ni mtumishi wa serikali kada ya elimu (mwl)


Sababu hasa ni hizi

1. Interest au hob

Kiukweli hii kazi siipendi niliisomea bada ya kuwa sina otenative najitaidi niikubali but inashindikana so naona kama napoteza muda


2. Kipato

Najua kuwa watumishi weng hasa awamu hii ya 5 weng wanalalamika hali ya uchumi but mmi naona hii yangu ni too much


Kiukweli najitahidi sana kujibana ila naona nashindwa, nashindwa kufanya hata mambo ya kawaida tu nikiwa kama baba natamani familiar yangu angalau iishi standard hata kiasi tu but huku nliko naona kama ndoto

Yan labda uwe mzee wa topup jambo ambalo naona pia ntaongeza ufukara mana ukiisha ndo utataabika kama nnavyoona wengine


Lengo la uzi huu ci kuwatangazia msimamo wangu bali ni kuwaomba wale ambao walishachukua maamuzi kama yangu au wanaotarajia hivyo waendlee kunipa moyo pia wote ambao watakua na wasaa basi wanisaidie kimawazo nifkie lengo langu


Naomba kuwaslisha


NB: Pls nmejitaidi kutumia lugha nzuri naomba bro o sister kama unanishaur bas lugha iwe ya kunielewesha isiwe ya kebehi au kunitusi kwan kuyaheshimu maamuzi ya mtu ni jambo la busara


 
 
Back
Top Bottom