Mradi mdogo wa nguruwe

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Banda la kutosha nguruwe wa 5 kitaalamu linaweza gharimu Tsh 741500/= (makadilio ya juu)


GHARAMA ZA GURUWE 5

Guruwe wa miezi mitatu anauzwa 1@60000

Kwa nguruwe 5 *60000 = Tsh 300000/=

GHARAMA ZA CHAKULA

Gharama za chakula kwa nguruwe wamwanzo 5 kwa miezi 3


Nguruwe hukuwa kwa kipindi cha miezi 6 hadi kufikia uwezo wa kupandwa


Nguruwe mmoja = kg 2/kwa siku


Nguruwe 1 kwa miezi 3 = 2 kg x siku 90 = 180 kg


Nguruwe 5 kwa miezi 3 = 180 kg x 5 = 900kg


Gharama za chakula kwa kipindi cha mimba


Nguruwe hupeba mimba kwa siku 114


Nguruwe mwenye mimba hula 3kg ya chakula kwa siku


Nguruwe 1 = 3 kg ya chakula kwa siku


Nguruwe 1 kwa siku 114 = 3 kg x 114 day = 342 kg za chakula


Nguruwe 5 = 342 x 5 = 1710 kg


Gharama za chakula kwa nguruwe 5 wazazi na watoto


Nguruwe anae nyonyesha atakula 5 kg kwa siku (hii ni makadilio ya nguruwe mwenye watoto 5)


Inapatikana kwa:

Jumla ya chakula cha mama ujumlishe na 1/3 ya chakula watachokula watoto wote


Kwa siku 56 = 5 kg x 56 = 280 kg

Kwanguruwe 5 = 5 x 280 kg= 1400 kg


JUMLA utaitaji


4010 kg za chakula hadi watoto wakue


Ngunia moja la pumba la debe 6 lina 70 kg


(kumbuka nguruwe ni mnyama anaekula kila kitu binadamu anachokula)


Jumla ya gharama za chakula itakua 400000/=

(gharama hii inaweza badilika kutokana na eneo)


GHARAMA ZA CHANJO NA MADAWA

Deworming / minyoo- ivemic 12000/=

Madini ya iron wakati wa ujauzito -iron injection 15000/=

Vitamin- multivitamins 5000/=

Vidonda- woond spry 9000/=

Iodine – 3000/=


JUMLA NI TSH 44000/=


(izo ni dawa na chanjo muhimu na bei yake itategemea sehemu uliyopo)


GHARAMA ZA ENEO

Kama unaeneo lako hii itaokoa kiasi kikubwa cha pesa wakatu wa kuanzisha mradi.

(kumbuka ni vyema eneo lako liwe mbali na makazi ya watu)


MAKADILIO YA FAIDA KWA MZAO WA KWANZA


Toa jumla ya gharama zote ulizotumia na mapato


Nguruwe huzaa kuanzia watoto 5 na kuendelea. Kwa makadilio ya nchini kwa majike matano ya nguruwe kunauwezo wa kupata nguruwe watoto siyo chini ya 25 kwa mzao mmoja. Nguruwe mwenye umri wa miezi 6 huweza kuuzwa au kuchinjwa kwa ajili ya nyama


Kuuza kwa jumla akiwa mzima >

Ndani ya watoto 25 unauwezo wa kuuza nguruwe 20

Nguruwe mmoja huweza kuuzwa 370000,

370000 x 20 = 7, 400, 000

Kuuza kama nyama

Nguruwe wa miezi 6 unauwezo wa kupata nyama kilo 90

Kilo 90 kwa nguruwe 20 ni kilo 1800

Kwa makadilio ya chini kilo moja ya nyama ya nguruwe huuzwa shilingi 6000

Kilo 1800 x 6000 = 10, 800, 000


(kwa maeleza zaid ya Ufugaji wa aina yeyote karibu)


Sent using Jamii Forums mobile app


 
 
Back
Top Bottom