- Joined
- Mar 14, 2026
- Messages
- 33,422
Nimeshindwa kuelewa niiweke wapi thread hii baada ya kusoma makala moja pale Mwanachi kuhusu mada ambayo imekuwa inakera akili yangu muda mrefu sana. Thread ingeweza kuwa siasa, uchumi au kwenye falsafa; nikaamua kuiweka hapa kwenye falsafa.
Nimekuwa na bahati sana ya kutembea na kuishi katika nchi nyingi sana duniani, ila sijawahi kufika nchi ambako biashara zote zinafanyika katika dola za kimerakni zaidi ya marekani kwenyewe. Hata Kanada ambayo ni jirani kabisa na marekani na raia wake wanafanya manunuzi yao sehemu yoyote ya mpaka, ukishavuka kuingia Canada unatumia Canadian Dollar, na ukirudi Marekani unatumia American Dollar.
Je kinachotusumbua Watanzania ni ulimbukeni au kweli ni udhaifu wa sarafu yetu? Nimeangalia trends kwa muda wa miaka kumi kuhusu mabadiliko ya thamani ya sarafu mbalimbali dhidi sarafu ya kimarekani na kugundua kuwa sarafu yetu ni stable kiasi cha kutosha, kwani haijawahi kubadilika ghafla ghafla. Ingawa kuna nchi nyingine kama Kenya na South Afrika zilikuwa stable zaidi yetu lakini mabadiliko ya sarafu ya Tanzania hayajawa so alarming kiasi kuwa biashara zetu tuziendeshe kwa hela ya kigeni; nikitoka Tabora na hela yangu ya madafu siwezi kulala hoteli za maana Tanzania mpaka ninunue dola za kimarekani na kumpa faida muuzaji wa dola hizo kabla sijampa faida mtu wa hoteli, je hiyo kweli halali kwa nchi?
Chini hapo nimeweka trends zinazoonyesha jinsi sarafu mbalimbali zilivyobadilika katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Ingawa sarafu ya Tanzania imekuwa inapoteza thamani, upotezu huo ni kwa currency investors tu wanaoinvest kwa muda mrefu kwani hauathiri kabisa katika biashara za kila siku kwa vile thamani hiyo ilikuwa inapotea kidogo kidogo. Mabadiliko ya thamani ya sarafu ya kitanzania hayatofautiani kabisa na yale ya sarafu ya Botswana lakini mpaka kesho hutakuta Botswana wanaendesha biashara ya ndani kwa kutumia dola ya kimarekani. India vile vile mambo ni hayo hayo.
Wataalamu wa mambo ya pesa mtusaidie kwenye tatizo hio.
Sarafu ya Tanzania
Sarafu ya Kenya
Sarafu ya Afrika ya kusini
Sarafu ya India
Sarafu ya Botswana
Sarafu ya Canada