Kama unasumbuliwa na mbu au mtaa wenu kuna mbu soma hapa na upate fursa ya kujiingizia kipato

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU


MALIGHAFI

1. PARAFFIN WAX

2. STERINE

3. BORIC ASID

4. MOULD(MAUMBO)

5. UZI (UTAMBI)

6. RANGI KAMA UKIPENDA

7. JIKO

8. SUFURIA


MAANDALIZI

Andaa maumbo ya mshumaa kwa Jinsi unavopenda unaweza kutumia bati


Andaa utambi kwa kuchukua boric asid vijiko vitano vya chakula changanya Na maji vijiko vinne vya chakula, koroga kwa muda wa dakika tano, KISHA toa Na ANDIKA ili ukauke, sababu ya kufanya hivi ili utambi usiishe haraka wala kutoa moshi. Na hii ndiyo Kazi kubwa ya boric asid


UANDAAJI WA MSHUMAA


Baadavya kuwa umeandaa maumbo Yako ya mshumaa chukua utambi wako Na uweke katikati ya mould Yako KISHA funga utambi wako juu ya chombo chako kwa kushikiza Na kijiti. Kijiti kitakusaidia ili utambi usikae pembeni


Washa jiko Lako Na weka sufuria Yako jikoni chukua paraffin wax kilo moja, sterine vijiko vinne, rangi kijiko kimoja cha chai, perfume kama ukipenda kijiko kimoja cha chai


Wakati mchanganyiko wako unayeyuka koroga taratibu mpaka uchanganyike vizuri


Epua mchanganyiko wako Na anza kuweka kwenye maumbo Yako uliyoandaa kwa kuweka utambi ndani yake


Weka sehemu ya kivuli ili mshumaa wako upate kuganda kwa urahisi ukisha ganda utoe taratibu kutoka katika hayo maumbo yake _BAADA YA HAPO MSHUMAA UTAKUWA TAYARI KWA MAUZO NA MATUMIZI YA NYUMBANI


NB: SIMPRONELLA/CITRONELLA hii ni perfume Na pia ni dawa ya kuua mbu ko kama ukipenda mshumaa wa kuua mbu basi sehemu ya kuweka perfume weka aina hii


Ahsante kwa maswali Na ushauri wa maswala ya ujasiriamali usisite kutupigia Simu Namba 0743550599


Au tuandikie kwenye e-mail


Maoningalla@gmail. Com


Kwa ajiri ya Kupata VITABU vya uandaaji wa BIDHAA MBALIMBALI ZA VIWANDANI KWA NJIA RAHISI NA ZENYE UBORA UNAOTAKIWA


 
 
Back
Top Bottom