Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP)

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Awali: pongezi kwa wote wanaohusika na mradi huo wa kuboresha Jiji la Dar es Salaam.


Pili: Wahaya wana msemo: ukienda kuomba maziwa, angalau basi uje na Kihansi (kibuyu).


Tatu: Barabara nyingi zimejengwa vema kabisa, kwa kiwango cha lami. Barabara hizo zinaachiwa kujaa michanga. Baada ya kusaidiwa kujengewa barabara za mitaa, wananchi tusisubiri "washirika wa maendeleo" watakaokuja kutusaidia kufagia barabara zetu. Tukumbuke, michanga ikiachiwa barabarani, barabara huwa na mashimo na baadaye kuharibika zaidi. Kama barabara zimejengwa Kwa hisani ya watu wa..., Hata kuzifagia? "Ng'ombe" hatuna, tumeenda kuomba 'maziwa'; hata kibuyu cha kuyabebea? Wejemeni..!


 
 
Back
Top Bottom