Baada ya machinga wa kichina kutakiwa kuondoka Tz, ubalozi wa China wapiga stop viza

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Haya ni maajabu, Baada ya serikali kutangaza ktk vyombo vya habari kuwa machinga wa kichina waondoke, Ubalozi wa china umepiga stop viza kwa raia wote wa Tanzania wanaotaka.


Yaani hawa wachina tayari walishaona ni haki yao kuvunja sheria!! Kweli T. I A. Yaani wataka kulazimisha wafanye biashara kinyume na sheria!!


Hivi huyu waziri wetu tuliyempa dhamana ya kushughulikia mambo haya ina maana hana taarifa.


Taarifa za uhakika ni kwamba pale hong kong Watanzania wanataabika hakuna viza za china na huu ni mwezi wa 4 unakatika, hakuna aliyefanikiwa kupata viza


Ubalozini kwao pale Dar es Salaam pia hawatoi viza labda uwe mtu wa serikali. Sasa kama huu ni utaratibu mpya kwa nini wizara isiwatangazie Watanzania kuwa utaratibu wa kwenda china umebadilika kuliko kuwaacha watu wakitaabika na kupoteza muda ubalozin i, Huu ni ujinga. Waziri anayehusika anasemaje,


 
 
Back
Top Bottom