Vitu vya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara ya spea za magari madogo

PamojaForums · Sep 5, 2026 at 5:17 PMReplies 0 · Views 0
#1
Habari,


Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, naomba mwenye ujuzi wa biashara ya Spea za Magari madogo ya kutembelea hasa Toyota (IST, Raum, Spacio, Carina, GX 100 n. K) anisaidie mambo muhimu ya kuzingatia kwa ninaetaka kuanzisha biashara hii.


Mfano aina ya spea zinazotakiwa kwa sana, muuzaji wa spea za jumla na original na mwenye bei nafuu, spea gani muhimu kwa mara ya kwanza kuweka dukani na vinginevyo muhimu.


Mahali ninapotaka kufungua ni mkoani nyanda za juu kusini. Msaada wakuu ikiwezekana na namba za supplier,


Tapeli usije DM tafadhali.


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread