Ushauri wa bure kwa Imani Kajula... THE VIBE CLUB.

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 11:06 AMReplies 0 · Views 0
#1
The VIBE CLUB iliyopo jijini Mbeya eneo la Forest jirani kabisa na Chuo Kikuu cha Mzumbe-Tawi la Mbeya, Ni Club ya kisasa na ya aina yake eneo lote la nyanda za juu kusini Tanzania (Rukwa Mbeya, Ruvuma, Iringa, Njombe na Katavi unaweza kuifananisha na

Maisha Club, Sunsiro Club na Bilicanas-Dar

Club 84-Dodoma

La Liga-Moshi

La Cassa Chica-Tanga

Lakini Club hii inayomilikiwa na kijana ambaye amebobea Masoko katika (Marketing) Imani Kajula na yenye wafanyakazi weledi, usalama wa uhakika, mazingira bora, usafi wa hali ya juu na yenye madaraja(Class) yaani VIP na kwa kawaida... Haina wateja kabisa ukizingatia ilikuwa Ijumaa (Kulikuwa na wateja 10 tu) (VIP wateja 2) ukilinganisha na Pamodzi... Club chafu sana, Vyoo vichafu, Giza, vurugu sana, Hakuna ulinzi baadhi ya wateja walikuwa na visu na BastolasalamaHakuna Emergency exit ukitokea moto ndiyo hivyo tena... Ikiwa na wateja waliojaa mpaka hata hakuna pakukanyaga, hewa ni nzito...(Wateja zaidi ya 200)


Ushauri wangu kwako Bw. Kajula

Badilisha Dj

Tambulisha huduma ya Ladies Free on weekdays

Puguza Kiingilio Badala ya Elfu 5 cha sasa kiwe Elfu 3

Kiingilio cha Partners kiwe Elfu 5

Punguza Bei ya Vinywaji

Kampuni Corporate zilizopo hapo jijini Wafanyakazi wake waingie kwa Entries ya Shilingi Efu 1 kila mmoja ilimradi atoe kitambulisho.

Anzisha Members Coupons nk nk...

Natumaini utalifanyia kazi wazo langu... Kwani najua unapita humu...


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread