Tupeni mrejesho mliowekeza kwenye mashamba ya miti

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 1:56 AMReplies 0 · Views 4
#1
Habari za jioni wakuu,

Kumekuwa na threads nyingi sana hapa JF kuhusu uwekezaji kwenye mashamba ya miti kwa ajili ya mbao.


Naamini wako wengi waliovutiwa na uwekezaji huu wa muda mrefu ambao umekuwa ukinadiwa kuwa na tija sana kwa miaka ya hivi karibuni.


Basi leo nikaona siyo vibaya kufungua thread hapa ili kuweza kupata uzoefu na mrejesho kupitia members wengine ambao walishawishika kufikia hatua kwenda kuwekeza kwenye uwekezaji huu.


Naamini wengi tungependa kujua hatua mlizopitia mpaka kufanikisha/kutokufanikisha katika uwekezaji huu.

Karibuni sana kuchangia wadau.


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread