Tanzania private sector foundation (tpsf)

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 11:06 AMReplies 0 · Views 0
#1
Wapendwa wana JF,


Asalaam Aleykum/Bwana Yesu apewe sifa.


Natumai wote mu wazima wa afya.


Mimi ni mjasiliamali, katika pita pita zangu nilikutana hii kampuni (TPSF) ikitoa grant kwa wafanya biashara waliosajiriwa kihalali wakubwa kwa wadogo.


Mwaka 2009 nikapewa grant ya millioni 15 ambayo imeniwezesha kufanya mambo makubwa na kujiendeleza ki biashara.


Sasa basi wamerudi na miradi ifuatayo:


Wale wenye miradi ya Tours, Food processing na Natural Resources sasa hivi ndiyo wanapewa GRANTS kuendeleza biashara zao. Mimi kama mwanaharakati nimeona ni vizuri tushirikiane ili wale wenye nia nao wakafaidike kama nilivyofaidi mimi.


Ofisi zao ziko Mwaya Road, Masaki. Ukifika pale utapata information na kitu gani ufanye. Nimeona na tangazo lao TBC1 jana.


Kila la kheri.


CD


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread