Na Bishop Hiluka
(Mwandishi wa stori za kusisimua zilizowahi kuchapishwa hapa JF za Kizungumkuti!; Laiti Ningejua!; Hekaheka!; Hadi Lini! Na nyinginezo)
0685 666964
SAA 1: 35 asubuhi, Samuel Kambona alishuka kutoka ndani ya gari aina ya Toyota Alphard la rangi ya bluu katika viunga vya maegesho ya magari vya majengo ya hoteli ya Udzungwa Beach Resort, iliyopo katika ufukwe wa Oystebay, jijini Dar es Salaam.
Gari lile lilikuwa na nembo ubavuni iliyokuwa na maandishi ya Udzungwa Beach Resort.
Samuel maarufu kama Sammy, alikuwa kijana mtanashati mwenye umri wa miaka 35 na msomi wa Shahada ya Umahili ya Biashara za Kimataifa na Lugha (M. A in International Business with Languages), aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Warwick Nchini Uingereza,
Alikuwa mrefu na mweupe mithili ya chotara wa kizungu, mwenye sura ya tabasamu muda wote. Urefu, mwili wake wa kimazoezi, utanashati na asili ya ngozi yake nyeupe ni vitu vilivyowavutia wasichana wengi aliokutana nao.
Ukiongezea na ndevu nyingi alizopenda kuzinyoa katika mtindo wa Circle beard au kama wengi walivyozoea kuita “O”, vilimfanya azidi kuwa mvuto mkubwa kwa walimbende pindi walipomtia machoni.
Siku ile ilikuwa Ijumaa, kama kawaida yake, Sammy alikuwa katika mwonekano maridadi kabisa, akiwa amevalia shati zuri la rangi ya samawati la kitambaa brandi ya Barba ndani ya suti nyeusi ya aina ya Dunhill, tai ya rangi ya bluu shingoni na viatu ghali vya ngozi halisi kutoka nchini Switzerland.
Pia alikuwa amevaa saa ya mkononi aina ya Cartier iliyokuwa na nakshi ya madini ya dhahabu na kujipulizia manukato ghali aina ya Dolce & Gabbana. Mkononi alikuwa amebeba mkoba wake mdogo wa kiofisi aina ya Pad & Quill wa rangi ya hudhurungi.
Wakati akishuka kutoka kwenye gari manyunyu mepesi ya mvua yalikuwa yakianguka ardhini, lakini bado hayakumzuia Sammy kutembea taratibu akikatisha kwenye viunga vya maegesho ya magari na kuelekea mbele ya jengo la mbele la ile hoteli ya kitalii yenye hadhi ya nyota tano.
Wakati akitembea macho yake yaliangaza huku na kule kana kwamba alikuwa akitafuta kitu. Alipishana na askari mmoja wa ulinzi kutoka kampuni ya ulinzi ya Spark K7 Aliyekuwa akilinda eneo lile la viunga vya maegesho ya magari.
Eneo lile lilikuwa pana likiwa na uwezo wa kuruhusu magari madogo hadi 100 kuegeshwa kwa wakati mmoja, na lilikuwa limepandwa miti mirefu ya kivuli aina ya ‘Quercus virginiana’ na ‘Arecaceae’ iliyojulikana pia kama ‘Coconut palms’.
Pia eneo lile lilipandwa nyasi nzuri laini aina ya ‘Citronella’ na kulikuwa na bustani ya maua ya kupendeza yaliyotoa hewa safi ya upepo wa asili baina ya sehemu moja ya maegesho ya magari na sehemu nyingine, ndani ya uzio wa yale majengo ya hoteli.
Kwa yeyote aliyefika Udzungwa Beach Resort angeweza kubaini mara moja kuwa majengo ya hoteli hiyo yalijengwa kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kulikuwa na majengo makuu mawili, moja lilikuwa mbele na la pili lilikuwa nyuma na kila moja lilikuwa na ghorofa saba za juu na mbili za chini, zilizotumika kwa ajili ya kumbi za burudani, kumbi za mikutano na migahawa ya kisasa ya chakula cha kitanzania na cha kimataifa. Pia kulikuwa na maduka na ofisi za utawala kwenye orofa ya chini nay a kwanza ya jengo la mbele.
Katika eneo lile kulikuwa na duka kubwa la bidhaa mbalimbali maarufu kama “Supermarket”, duka kubwa la vipodozi na nguo za kisasa (Boutique), na duka la kubadilishia fedha za kigeni maarufu kama “Bureau de Change” na vyumba viwili vidogo vyenye Mashine za ATM
Pia kulikuwa na jengo maalumu la klabu iliyojulikana kama Paradise Club, ambayo ilikuwa kwenye jengo la nyuma iliyowakutanisha mabilionea na baadhi ya vigogo serikalini na ilikuwa na ulinzi mkubwa sana, nje na ndani ya klabu.
Walioruhusiwa kuingia ndani ya klabu hiyo ni wanachama tu waliokidhi vigezo na kusajiliwa, ambao walilipa kiasi kikubwa cha ada ya uanachama kila mwaka.
Ndani ya majengo yote ya hoteli hiyo kulikuwa na kamera za usalama (CCTV) kila kona, viyoyozi vilivyosambaa kila mahali, na kutoka ghorofa moja kwenda nyingine kulikuwa na ngazi za kawaida na vyumba maalumu vya lifti za kisasa. Pia kulikuwa na ngazi iliyoendeshwa kwa umeme.
Yale majengo yalijengwa katika eneo tulivu mno lisilo na bughudha la ufukwe wa Oysterbay, jirani kabisa na ofisi za kibalozi na makazi ya watu wenye ukwasi, takriban kilomita tatu tu kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa watu wengi wenye ukwasi, Udzungwa Beach Resort ilikuwa ndiyo sehemu nzuri na tulivu zaidi ya kwenda kujipumzisha na kufurahia maisha, kwani ilikuwa imezungushiwa uzio madhubuti wenye ulinzi na kamera za usalama ulioifanya kuwa mahali patulivu zaidi na pa usalama wa uhakika.
Asubuhi ile kulikuwa na magari machache madogo na mabasi mawili ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Cape Town cha nchini Afrika Kusini na Chinhoyi cha nchini Zimbabwe yaliyokuwa yameegeshwa katika viunga vya maegesho ya magari.
Pia kulikuwa na malori mawili makubwa ya kubebea watalii wa masafa marefu aina ya Mercedes Benz, yaliyokuwa yameegeshwa mwisho kabisa wa yale majengo.
Mbele ya ile hoteli katika jengo la mbele Sammy aliipita milingoti saba iliyokuwa na bendera za Afrika Mashariki, Marekani, Uingereza, India, China, Afrika Kusini na bendera yenye nembo ya Udzungwa Beach Resort, zilizokuwa zinapepea taratibu.
Kulikuwa na mlango mkubwa wa vioo mbele ya jengo na varanda pana yenye ngazi iliyofunikwa kwa kofia nzuri ya zege ikiwa na sakafu nzuri yenye marumaru iliyonakshiwa kwa maandishi ya “Udzungwa Beach Resort”.
Kijana mmoja askari wa kampuni ya ulinzi ya Spark K7 Alikuwa amesimama kikakamavu kwenye ile varanda pana akiwa kando ya ule mlango mkubwa wa vioo wa kuingilia ndani. Yule askari wa ulinzi aliyeitwa Fred Luvanda alimuona Sammy na kumpokea kwa tabasamu la kirafiki lililokuwa na bashasha zote kwenye uso wake.
Endelea kufuatilia...
SEHEMU 2
SEHEMU YA 3

No reactions yetReply / React