Mwekezaji anatafuta shamba

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 11:05 AMReplies 0 · Views 0
#1
Salamu wakuu!


Naomba mchango wenu kimawazo maana nina muwekezaji anatafuta shamba kubwa maeneo ya Morogoro. Angependa sehemu inayostawisha machungwa, malimao, machenza (Citrus) na mananasi. Pia Iringa kwa ajili ya ngano, matunda na mboga.


Wataalamu, wenye uzoefu na wenye contact naomba ushauri wenu. Tunahitaji kujua shamba liko eneo gani, ukubwa, bei, jinsi panavyoingilika, ukaribu wa maji, upatikanaji wa mvua na masharti ya uuzaji. Lengo ni kuwekeza kwenye kilimo kwa muda mrefu na hata mikataba itajali maslahi ya majirani na wanavijiji.


Shukurani.


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread