Msaada Wa Mawazo, Mtaji Mil 1 Nafikiria Kuanza Biashara Moja Kati Ya Hizi....

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 10:54 AMReplies 0 · Views 3
#1
Salam za dhati kwenu wakuu!


Mimi kama kijana nina nia ya kweli,

Kwa mtaji mdogo nilio nao, nimefikiria kufanya moja kati ya.... Kuuza na kusambaza kuku wa kienyeji /magunia ya mkaa ktk hotel mbalmbal hapa dar


Kabla ya maamuzi tafadhali nishaurin ipi naweza anza nayo kwa hapa DAR

Pia naomba kwa yeyote mwenye kujua lolote kuhusu vp na mkoa gani naweza pata kuku wa kienyeji kwa bei nafuu ya jumla

Pili vp kuhusu biashara ya mkaa, changamoto na namna gani naweza pata mtu wa kuniletea kwa bei ya jumla toka porin ili nami niuze hapa dar kwa bei nafuu kidogo?


NB: nakaribisha mawazo na ushauri kama kuna biashara mbadala mtakayoona ninyi inafaa zaid ya hizo!

Ahsanteni sana na karibuni sana!


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread