Msaada kufungua duka la nafaka Jumla na Reja reja

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 1:54 AMReplies 0 · Views 0
#1
Habari

Mimi si muandishi sana humu lakini ni msomaji mmbobezi, muajiliwa toka 2008.

Katika maisha yangu sijawahi kufanya Biashara yoyote au shughuli yoyote ya kuniingizia kipato zaidi ya Mikopo bank na Ujira wa mwisho wa mwezi.

Hivi Karibu nimapata wazo la kufanya Biashara au kilimo. Kama kichwa kinavyosema naombeni mwenye ujuzi wa kuanzisha Biashara ya Nafaka kwa Jumla na reja reja,. Hivi Karibu Natarajia kupata kiasi flani cha kuanzia Kwani Kuna vikoba vya wife turijiweke akiba huko kanisani tutavunja.

Mwenye ujuzi kwenye point zifuatazo

1. Upatikanaiji wa nafaka

2. Vibari husika,

3. Upatikanji wa Faida na Hasara zake

4. Kiasi cha mtaji cha kuanzia

5. Hiana za nafaka Zenye Faida


Kumbuka haswaa malengo yangu Mchele, Maragwe, Soya, Mtama, Mbaazi, Kunde, Mahindi, Choroko nk...


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread