Mbuzi wa barafu wanaweza kuuzika Tanzania?

PamojaForums · Sep 5, 2026 at 5:17 PMReplies 0 · Views 0
#1
Mbuzi ni mnyama anae lika sana Tanzania, kwa sherehe za kifamilia au hata social gatherings mfano birthdays, kutoa mahari, ubatizo nk. Pamoja na hayo mbuzi choma ni kitafunwa pendwa kwa wanaokunywa pombe na wasiokunywa pia.


Wengi tunanunua mbuzi na kumtafuta mchinjaji. Anachinjwa mbuzi saa 11 alfajiri na saa mbili watu wakunywa supu ya utumbo.


Kuwa na machinjio ya mbuzi kwa ajili ya kuuza walioganda. Wateja watapatikana kweli? Hapa tunaongelea mbuzi alietolewa utumbo, kichwa na miguu.


Kwa wale wanaotaka sehemu tu mguu pia unaweza kupatikana.


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread