Makosa 5 Wajasiriamali Wanafanya Katika Mtandao wa Facebook na Instagram

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Kama wewe ni mjasiriamali unayetafuta wateja kupitia mtandao wa Facebook na Instagram lakini unahangaika basi inawezekana unafanya makosa yafuatayo:


  1. Unatangaza bidhaa / huduma unazotoa: Mitandao ya kijamii (tofauti na e-commerce) hayakutengenezwa kwa ajili ya watumiaji kununua bidhaa / huduma yoyote. Facebook na Instagram ni vijiwe vya watu kukutana, kuchat na kufuatilia umbea.
  2. Unatumia ma group ya Facebook kutangaza bidhaa/huduma zako: Japokuwa Facebook wana ma group ya biashara haimanishi kuwa ukitumia group hizo utapata wanunuzi wa kununu bidhaa huduma unazotoa. Tatizo kubwa la ma group ya Facebook ni kuwa wauzaji ni wengi kuliko wanunuzi. Utajikuta unaingia katika competition bila ya sababu yoyote.
  3. Unatangaza Biashara Yako Katika Kurasa Binafsi: Badala ya kutumia Facebook business page, unatumia personal page (kurasa binafsi) kutangaza bidhaa na huduma unazotoa.
  4. Huwekezi katika matangazo: Kwa vile wajasiriamali wengi wanaogopa kupoteza pesa (na kuona pesa za matangazo kama matumizi badala ya uwekezaji) wengi hawathubutu kutumia pesa zao kutangaza. Kosa kubwa.
  5. Una boost matangazo: Najua unaweza kushanga kwanini ninasema ku boost matangazo ni kosa. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa ku boost matangazo yanaleta tija kwa muda mfupi sana na baada hapo gharama za matangazo yanakuwa juu. Cha kufanya ni kuweka matangazo yako katika Facebook Ads Manager (Se connecter à Facebook | Facebook). Matangazo yatakuwa rahisi na kila ukiongeza bajeti yako matangazo yako yataonekana kwa watu wengi na kukuletea matunda makubwa zaidi.
Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Mtandao wa Facebook na Instagram Kunasa wateja na jinsi nilivyoweza kutengeneza hadi Tshs. 945, 000 kwa siku Bofya hapa.


Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,


Dr. Said Said


 
 
Back
Top Bottom