Kumbe ni kweli kuwa zembwera ni kilaza!! Hata hili 2 hajui!

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 11:04 AMReplies 0 · Views 3
#1
Nakubaliana na wale wadau wa jf waliokuwa wanadai kuwa mtangazaji wa east africa radio maarufu kama zembwera ktk kipindi cha super mix, ni kilaza kwani hajui hata vipimo vya urefu! Juzi anasema alishuhudia mtoto amegongwa na gari na kuburuzwa umbali wa kilomita 150!! Na hakufa! Sawa na urefu wa viwanja vi 5 vya mpira wa miguu!! Hivi viwanja viko dunia ipi? Vyenye urefu huu! Tena anarudia rudia kwa msisitizo, kuonyesha kuwa anajua kile anachoongea, na hata huyo mtangazaji mwenzake michael baruti kumsahihisha hamna! Jamani hata ile kanuni ya darasa la 4 ya mimi sili dagaa maana dagaa huleta kichaa, ilimpita kushoto! Kwa watangazaji hawa bado kuna safari ndefu.


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread