Kitabu cha "dr. Slaa mjenzi makini wa taifa" kinawakawaka channel ten leo jioni

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 11:07 AMReplies 0 · Views 0
#1
Channel ten leo jioni imeonyesha uzinduzi wa kitabu kiitwacho "Dr. Slaa mjenzi makini wa Taifa."


Kitabu hicho kinazungumzia mchango wa Dr. Slaa katika ujenzi wa taifa hili changa.


Utoaji wa vitabu vya aina ya "memoirs" ni jambo la kawaida sana ikumbukwe Barrack Obama alitoa kitabu cha "Dreams from My father" na "The Audacious of Hope" ambavyo vilisaidia sana kumweka kwenye chati katika chaguzi za nchi hiyo.



Kwetu hapa watu hawana tabia ya kujisomea vitabu, hivyo ufanisi wake kwenye kampeni hii unatarajiwa kuwa ni kiduchu ukilinganisha na mchango mkubwa utakaojitokeza kwenye kampeni zake ambazo zinakwenda vizuri mno kuliko matarajio ya wengi.



Kama kitabu hicho kitawekwa kwenye internet basi wengi tutaweza kukisoma kabla ya uchaguzi au kama watakisambaza mapema mikoani itasaidia kwa haswa sisi wapashaji watu wengine habari.


Kitabu hicho kimehaririwa na mwandishi wa siku nyingi Bw. Henri Muhanika.


Mara nitakapokisoma kama itakuwa kabla ya uchaguzi nitakichambua kwa manufaa ya wale ambao hawataweza kukisoma kwa sababu moja au nyingine



 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread