CV ni zaidi ya orodha ya shule ulizosoma; ni chombo cha masoko (marketing tool) kinachomshawishi mwajiri kuwa wewe ndiye suluhisho la matatizo yake. Ili uweze kushindana, wasifu wako lazima uwe wa kisasa, wenye mpangilio mzuri,na unaoweza kusomwa kirahisi na mifumo ya kidijitali (ATS – Applicant Tracking Systems).
Hapa unaweka jina lako kamili, namba ya simu, na anwani ya barua pepe inayofanya kazi.
Haya ni maelezo mafupi ya aya moja yanayoelezea wewe ni nani, ujuzi wako mkuu, na nini unaleta kwenye kampuni. Hii ndiyo sehemu ya kwanza mwajiri anayoisoma.
Orodhesha kuanzia elimu ya juu kuelekea chini (Reverse Chronological Order).
MUHTASARI WA KITAALUMA Mtaalamu wa [Taja fani yako, mfano: TEHAMA] mwenye uzoefu wa miaka [Taja idadi] katika [Taja eneo unalobobea]. Nina ujuzi thabiti wa [Taja ujuzi mkuu] na nimefanikiwa kusaidia [Taja mafanikio makubwa].
UZOEFU WA KAZI [Jina la Kampuni/Taasisi] | [Cheo Chako] [Mwezi/Mwaka wa Kuanza] – [Mwezi/Mwaka wa Kumaliza au Sasa]
Hapa unaweka jina lako kamili, namba ya simu, na anwani ya barua pepe inayofanya kazi.
Haya ni maelezo mafupi ya aya moja yanayoelezea wewe ni nani, ujuzi wako mkuu, na nini unaleta kwenye kampuni. Hii ndiyo sehemu ya kwanza mwajiri anayoisoma.
Orodhesha kuanzia elimu ya juu kuelekea chini (Reverse Chronological Order).
- Onyesha jina la chuo/shule, mwaka wa kuhitimu, na aina ya cheti ulichopata.
- Hakikisha taarifa hizi zinaoana na vyeti ulivyopakia kwenye mifumo kama Ajira Portal.
- Badala ya kusema: “Nilikuwa nikiandika ripoti.”
- Sema: “Niliandaa ripoti za kila mwezi zilizosaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwa 15%.”
- Hard Skills: Ujuzi wa kiufundi (mfano: Uhasibu, Programu za Kompyuta kama Excel, au Ufundi Mitambo).
- Soft Skills: Ujuzi wa kijamii (mfano: Uongozi, Mawasiliano, na Utatuzi wa Migogoro).
MUHTASARI WA KITAALUMA Mtaalamu wa [Taja fani yako, mfano: TEHAMA] mwenye uzoefu wa miaka [Taja idadi] katika [Taja eneo unalobobea]. Nina ujuzi thabiti wa [Taja ujuzi mkuu] na nimefanikiwa kusaidia [Taja mafanikio makubwa].
UZOEFU WA KAZI [Jina la Kampuni/Taasisi] | [Cheo Chako] [Mwezi/Mwaka wa Kuanza] – [Mwezi/Mwaka wa Kumaliza au Sasa]
- Mafanikio ya 1: [Elezea jambo ulilolifanya kwa namba au asilimia].
- Mafanikio ya 2: [Elezea jinsi ulivyoboresha utendaji kazi].
- [Jina la Chuo]: [Shahada/Diploma ya…], [Mwaka wa Kuhitimu].
- [Jina la Shule ya Sekondari]: [ACSEE/CSEE], [Mwaka wa Kuhitimu].
- [Jina], [Cheo], [Taasisi], [Mawasiliano].
- Jina Kamili: Vicent Mark Segona
- Anwani: S.L.P 1234, Kinondoni, Dar es Salaam
- Namba ya Simu: +255 712 000 000
- Barua Pepe: vicent@pamojaforums.com
- Namba ya NIDA: 19900101-12100-00001-20 (Muhimu kwa uhakiki wa uraia)
- Shahada ya Sayansi katika Teknolojia ya Habari (BSc. IT) – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), 2021.
- Diplomasia ya Elimu ya Sekondari (ACSEE) – Shule ya Sekondari Tambaza, 2017.
- Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) – Shule ya Sekondari Makongo, 2015.
- Nimesimamia ufungaji na matengenezo ya mitandao ya ofisi (LAN & WAN) kwa watumiaji zaidi ya 100.
- Nimefanikiwa kupunguza muda wa mfumo kukwama (downtime) kwa 20% kupitia maboresho ya kiufundi.
- Ninatoa msaada wa kiufundi (Technical Support) kwa wafanyakazi na wateja wa kampuni.
- Nilishiriki katika uhakiki wa mifumo ya usalama wa taarifa serikalini.
- Niliandaa ripoti za kila wiki kuhusu utendaji wa seva za ofisi.
- Ujuzi wa Kiufundi: Usalama wa Mtandao (Cybersecurity), Database Management (SQL), na Web Development.
- Ujuzi wa Lugha: Kiswahili na Kiingereza (Fasaha kwa kuongea na kuandika).
- Soft Skills: Uongozi wa timu, utatuzi wa migogoro, na uwezo wa kujifunza teknolojia mpya kwa haraka.
- Dkt. Anna Kilimali, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Simu: +255 754 111 222.
- Mhandisi Baraka Saidi, Mkurugenzi wa IT, Kampuni ya ABC. Simu: +255 655 333 444.
- Bi. Neema John, Afisa Rasilimali Watu, Mamlaka ya Serikali Mtandao. Simu: +255 784 555 666.
- Ukweli: Hakikisha taarifa zote unazojaza ni za kweli na zinaweza kuthibitishwa na vyeti vyako halisi (Original Certificates).
- NIDA: Usisahau kuweka namba yako sahihi ya NIDA kwani mfumo mpya wa Ajira Portal unaitumia kuhakiki taarifa zako moja kwa moja.
- Mpangilio: Tumia mpangilio rahisi kama huu (wa kuanzia uzoefu/elimu ya sasa kuelekea ya zamani) ili mwajiri apate taarifa muhimu kwa haraka.
- Kamilisha Wasifu (Profile): Hakikisha wasifu wako umekamilika kwa 100% kabla ya kuomba kazi.
- Namba ya NIDA: Hakikisha namba yako ya NIDA imehakikiwa kwani ni kiungo muhimu cha utambulisho wako.
- Nyaraka Halisi: Pakia vyeti halisi (Original Certificates) katika mfumo wa PDF kwani “Result Slips” mara nyingi hazikubaliki.
- Oanisha na Tangazo la Kazi: Angalia Job Categories (mfano: IT, Healthcare, au Education) na uhakikishe ujuzi uliouweka unaoana na kile mwajiri anachotafuta.