Huu ni ugonjwa gani? Tiba yake je?

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 11:06 AMReplies 0 · Views 4
#1
Katika pita pita zangu nimekutana na kijana wa takribani miaka 20. Na katika kujenga nae mazoea akaniambia kuwa, amekuwa akiumwa kichwa kila mwezi unapoandama. Na kabla ya kichwa kuanza kuuma hutanguliwa na kupiga chafya mfululizo.


Katika historia, mama yake ana matatizo ya ugonjwa wa kifafa. Aliponisimulia nilidhani labda na yeye amerithi tatizo la mamaye. Lakini nilipompeleka ktk hospitali ya mkoa aliambiwa kuwa hana ugonjwa huo.


Unaweza kuwa ni ugonjwa gani na tiba yale ni nini hasa!!


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread