Hivi kweli kuna biashara ya kuingiza faida kuanzia milioni 100 na kuendelea kwa siku/wiki/mwezi?

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 1:59 AMReplies 0 · Views 0
#1
Wakuu tushirikishane basi hizo biashara au madili ya biashara za kuingizia kiwango hiko cha faida kwa muda tajwa, hivi kweli zipo na kama zipo tushirikishane.


Mambo ya kufanya biashara kwa mazoea ni ya kijinga, miaka nenda rudi unaulizwa unajishuhulisha na nini, mtu anajibu, nafanya biashara, miaka 5, uko pale pale husogei, unafanya tu biashara, embu tushirikishane madili ya biashara zenye mipango ya kupiga kiwango hiko cha pesa kama faida.


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread