Wengi miongoni mwetu wamekuwa wakitaka kujua HISA ni nini, shauku hii imenifanya nidodose kidogo juu ya hisa kwa faida ya wengi. Kwa tafsiri lahisi HISA NI UMILIKI.
Mtu akisema nina hisa NMB anamaanisha ana miliki NMB. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida inayopatikana katika kampuni). Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake.
Mfano- Kampuni yaweza kuwa na hisa 1000, ikaamua kuuza hisa 500 na hisa 500 zikabaki akiba. Wale watakaonunua hizo hisa 500, wanakuwa wametoa mtaji kwa kampuni na kwa maana hiyo ndiyo wamiliki. Mwenye kuweza kununua hisa 251 atakuwa amenunua hisa nyingi zaidi kuliko yeyote na anakuwa na nguvu ya maamuzi katika vikao na gawio atapata kubwa kwa sababu ndie aliechangia mtaji mkubwa.
Faida za kuwa na hisa:
1. Unapata fursa ya kuwa mmoja ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ama moja kwa moja au kwa kuwakilishwa.
2. Mwanahisa anapofariki shughuli za kampuni haziwezi kuyumba kwa sababu jukumu la kazi za kila siku lipo mikononi mwa menejimenti
3. Ni lahisi zaidi kuuza HISA pindi unapoona hauhitaji kuendelea na umiliki
4. HISA ni dhamana (badala ya kuweka nyumba/shamba ili uweze kukopeshwa na taasisi za fedha waweza kuweka dhamana ya hisa zako)
5. Kampuni inapofanya vizuri sokoni ama kwa kutoa huduma/bidhaa bora au kwa kuwa na mipango mkakati mizuri thamani ya HISA hupanda. Wapo walionunua hisa za NMB tshs 600 lakini leo ni zaidi ya tshs 950.
Kwa maana hiyo mbali ya gawio mtu anaweza kuuza hisa kwa bei inayomlipa akilinganisha na bei ya kununulia.
NAOMBA NIKOMEE HAPA.

No reactions yetReply / React