Hii hali kwenye biashara siyo ya kawaida

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 1:49 AMReplies 0 · Views 3
#1
Mnamo mwezi wa nane mwishoni nilifungua biashara ya kuuza kuku Wa kukaanga pamoja na viungo vyake.


Wakati nimeanza mauzo yalikuwa hafifu ikawa hata elfu 5 haifiki ya mauzo, ndo nikaja na Uzi wa kuomba ushauri

Wakajitokeza waungwana wakanipa msaada wa mawazo

Miongoni mwao ni dada angu kutoka kigamboni (jina namhifadhi).


Alinipatia msaada mkubwa niliwahi kuelezea kwenye Uzi

Baada ya hapo mambo yakawa mazuri nikawa nauza sana yaani kwa siku nakaanga kama awamu 3 nauza wanaisha

Hali imeanza kubadilika wiki 3 zilizopita siuzi, unakuta nauza elfu 3 au sita.


Biashara yote inabaki kesho yake ukisema ni kuku Wa Jana watu hawanunui Sasa hivi mtaji naona unakata maana hakuna nnachoingiza


Nimeenda kwa mganga akanipa dawa za kuchoma na nyingine za kufukia ila wapi Hali inazidi kuwa mbaya


Nachanganyikiwa yaani


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread