Fremu ya biashara Dodoma mjini inahitajika haraka!

PamojaForums · Sep 5, 2026 at 5:17 PMReplies 0 · Views 0
#1
Wakuu nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya muungano!. Bila shaka mu wazima na kama una tatizo kidogo au sana la kiafya, basi natamka uponyaji kuanzia sasa, UPONYWE


Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu. Nahitaji fremu ya biashara inayofaa kwa biashara ya kuuza vifaa vya computer na simu pamoja na ufundi pia wa computer na simu.

Vigezo vya ukubwa wa fremu, siyo lazima iwe kubwa maana hata 3m kwa 4m inatosha kabisa.

Location ya fremu inazingatiwa zaidi maana biashara ni location kulingana na uhitaji. Hivyo inafaa iwe maeneo ya mjini ambapo wanafunzi na wafanyakazi wa maofisini wanapita zaidi bila kusahau raia wa kawaida.


Bajeti yangu ni wastani wa 300, 000/= kwa mwezi kulingana na vigezo hapo juu.


Natanguliza shukrani kwa wenyeji wangu wa dodoma katika kufanikisha adhma yangu.


Shukrani!


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread