Biashara ya Viungo (Spices)

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 1:50 AMReplies 0 · Views 0
#1
Jamani Habari Zenu.

Nilikuwa nataka kupanua wigo wa Biashaya ya Viungo(Spices). Nina duka dogo Zanzibar ila nataka niongeze wigo wa biashara.


Kwanza ninamalizia website yetu, ambayo itakuwa na maelezo yote. Natarajia kupost kwenye baadhi ya Local Magazine pia.


Nilikuwa nataka Mawazo yenu kwa mikoa ya hapa Tanzania ambayo biashara hizi au viungo hivi vinasoko zuri. Hata kama nchi za Jirani pia siyo mbaya maana sina Ideas kwa nje ya Znz


Viungo(Spices) ni kama zifuatazo:-

Cinnamon (Mdalasini)

Cumin (Uzile)

Ginger (Tangawizi)

Black pepper(Pilipili Manga)

Cardamon (Hiliki)

Lemons Grass (Mchaichai)

Cloves (Karafuu)

Vanilla (Vanila)

Nutmeg (Kungu Manga)

Turmeric (Bizari)

Coriander(Giligilani)

Fenugreek (uwatu)

Thyme(zahatari)


Spice Combination(Masala):-

Tea Masala

Fish/Meat Masala


Spices Gift Packs

-Oils Extracts

-Herbal Soaps


Na Je kuna Mikoa ambayo inalimazao lolote hapo juu kwa wingi. Na Idea ya kilo moja ni kiasu gani (Hii itanisaidia kama nitapata order kubwa, kujua wapi pa kuchukua)


Mbarikiwe

Naomba kuwasilisha,​


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread