Biashara ya baby diapers/ pampers almaarufu

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 1:49 AMReplies 0 · Views 0
#1
Habari wana jamvi wenzangu...

Baada ya kuona jambo hili na kuliangalia jinsi linavyoenda nimeona nilete kwenu kwa msaada wa zaidi. Nahitaji kwa mwemye uzoefu na biashara hii anisaidie mambo haya katika biashara ya dipers/ maarufu kama Pampers.

1. Supplier/ msambazaji wake mkuu ambae anauza bei za jumla

2. Bei zake. Na je zina faida kiasi gani. Mfano kama naanza na mtaji wa mil. 2

3. Sina shaka na marketing issue maana kila napopita naona zinaweza uzika bila tatizo (watoto ni wengi).

4. Yapi mabaya na hasara nazoweza pata katika mchakato huu?

5. Brand zipi zina soko sana na zinapendwa kutokana na unafuu wa bei na ubora wa bidhaa hiyo?


Tafadhali kwa mwenye ujuzi na biashara hii atumwagie data hapa.

Nawakilisha kwenu wadau.


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread