Bakari Mwapachu anyemelea uenyekiti bodi ya ATCL

Joined
Mar 14, 2026
Messages
33,422
Habari zilizozagaa mtaani ni kuwa Bakari mwapachu, yule mzee aliyeshindwa ubunge na Omar Nundu kule Tanga analobby Kikwete amteue kama mwenyekiti wa shirika la ndege la ATCL. Ukweli ni kwamba kama kweli hawa jamaa wanalitakia kheri shirika hili hawatathubutu kuchagua mwenyekiti wa bodi mchovu kama alivyo Mwapachu.


Makosa yalishafanywa huko nyuma kwa kumpa uenyekiti Mistapha Nyang'anyi sidhani kama Kikwete atakuwa na ujasiri wa kufanya makosa mara mbili baada ya vioja alivyofanya huyo bwana kuhusu kuwapeleka mahujaji Mecca!! Bakari hostoria ya utendaji wake haioneshi kuwa anaweza kuimarisha shirika la ndege; huyu bwana ni mtumiaji siyo mzalishaji.


 
 
Back
Top Bottom