Anguko la Ndugai: Somo la Katiba, viongozi na nchi

PamojaForums · Sep 6, 2026 at 2:01 AMReplies 0 · Views 5
#1
Hatimaye Spika aliyeongoza kwa 'mkono wa chuma'' anguko lake limetimia. Mh. Anaondoka akiacha historia ya Spika wa kwanza kujiuzulu tangu uhai wa Taifa hili


Spika asingeweza kutekeleza majukumu yake kwa fyongo yake na dhalili aliyopata Fyongo si alichosema ni kile alichofanya baada ya kusema. Hakusimama na kauli yake


Shinikizo la kuondoka lilitoka makundi ya jamii yakiona amepoteza imani au kudhalilika, Wapo wanaolaumu Mhimili wa serikali umeshinikiza Spika aondolewe


Inaweza kuwa ''kweli '' lakini kuna ubaya gani ikiwa mhimili hauwezi kufanya kazi na Spika? Ni Ndugai huyo huyo aliyewahi kusema ' ni lazima mihimili ifanye kazi pamoja''


Hoja si nani kashinikiza Spika ajiuzulu, hoja ni utaratibu uliotumika kumshinikiza aondoke


CCM ingeweza kumwita na kumlazimisha aondoke na angekataa ingechukua kadi. Spika anapigiwa kura na Wabunge ndivyo katiba inavyosema, wengi ni CCM


Ndugai aliamini kuishi kwa 'kupendelewa, mapenzi ya chama, kupendwa n. K.' na si katiba


Laiti katiba ingesema Spika haondolewi na chama baada ya kuchaguliwa Ndugai asingekuwa alivyo. Ndugai alitetea katiba mbovu iliyokuwa nzuri kwake leo Jan 06 ni shubiri


Mh Ndugai aliongoza harakati za ''kumdhalilisha'' CAG, kikatiba ana ulinzi wa kuondolewa. Ndugai hakuruhusu kuhoji utataribu kwa sababu alikuwa 'darling' wa CCM na serikali.


Mh alijisahau na kudhani ni mteule wa Mungu na si Mtanzania au mwanaCCM


Hili la Spika si kwamba linaonyesha matundu ya mihimili bali ubovu wa Katiba. Viongozi hujisahau wanapokuwa madarakani, wengi wamkuwa wahanga wa katiba hii


Wabunge na viongozi wa serikali ni watetezi wa katiba hii wakidhani itawalinda milele. Wasichojua ubovu wa katiba unawaathiri vizazi vyao vya leo kesho na keshokutwa


Anguko la 'mbabe' ni fundisho la kujenga misingi ya nchi inayolindwa kisheria na si fadhila. Watu wasilalamike mhimili mmoja kuwa na nguvu, waangalie namna ya kurekebisha nguvu hizo ki uwiano. Alipoondolewa CAG kibabe hakuna aliyejali.


Leo kaondoka Spika huku mhimili ''mwingine'' ukitiliwa shaka sana kama unatumika. Ni wajibu wa mihimili mingine kujijengea ulinzi wa kisheria kupitia Katiba yasijitokeze tena.


Malumbano hayana majibu isipokuwa jambo moja, mifumo yetu inahitaji marekebisho. Tume huru ya uchaguzi haitatupa majibu ya mifumo mibovu, leo kuna mtu ana majibu tofauti na jana! Tume huru ya uchaguzi haitaweka uwiano sawa wa mihimili


Leo tofauti na jana Mh Ndugai anaifikiria katiba zaidi kuliko tume huru ya uchaguzi


Tupitie maoni ya wananchi ya Rasimu ya Warioba tutengeneza utaratibu mpya-KATIBA. KATIBA ni msumeno unaokata mbele na nyuma, hauchagui siku wala tarehe


KATIBA ni nyaraka yetu, vyama ni mapito tu! Tutengeneze katiba inayojenga mifumo imara


Turudi kwa Mzee Warioba tudurusu nyaraka yake, maana kama ninyi viongozi msiojifunza fanyeni ziara Kongwa mtaelewa tunachosema


Tusemezane


 
No reactions yetReply / React
Continue the discussion on PamojaForumsOpen full thread